Loading...

Vigezo na Masharti

Karibu kwenye tovuti rasmi ya Hai Rural Teachers SACCOS (HRT SACCOS). Kwa kutembelea au kutumia tovuti hii, unakubali kufuata masharti na vigezo vilivyoelezwa hapa chini. Tafadhali soma kwa makini kabla ya kuendelea kutumia huduma zetu.

1. Uhakiki na Kubali

Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali kufuatana na kuzingatia Vigezo na Masharti haya. Ikiwa hutokubaliana na masharti yoyote haya, tafadhali usitumie Tovuti yetu.

2. Maelezo Kuhusu HRT SACCOS

Hai Rural Teachers SACCOS ni Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo kilichosajiliwa chini ya sheria za Tanzania na inayolenga kuhudumia Wanachama wake waliopo Hai na Siha na Wale Waliopo nje ya Hai na Siha. Bidhaa zetu za msingi ni:-

  • Hisa kwa Wanachama
  • Akiba kwa Wanachama
  • Mikopo kwa Wanachama
  • Akaunti za Amana kwa Wanachama

3. Usajili wa Wanachama

Usajili wa kua Mwanachama wetu unatofautiana na kutumia tovuti hii. Tovuti hii inaweza kukupa maelezo kuhusu usajili, lakini mchakato halisi wa kuwa mwanachama unahitaji kukamilika kwenye ofisi zetu na kufuata Kanuni na Masharti ya Chama chetu.

4. Faragha na Usalama wa Taarifa

Tunaheshimu faragha yako. Tafadhali soma Sera Yetu ya Faragha ili kuelewa jinsi tunavyokusanya, kutumia na kulinda taarifa zako binafsi.

5. Uwajibikaji wa Mtumiaji

Unakubali:

  • Kutotumia Tovuti yetu kwa madhumuni yasiyo halali
  • Kutoingilia kwa nia ya usalama wa Tovuti
  • Kusaidia kuhakikisha kuwa taarifa zote unazotoa ni za kweli na sahihi

6. Vikwazo vya Uwajibikaji

Tovuti inatolewa "kama ilivyo" na "kama inapatikana". HRT SACCOS haitoi dhamana yoyote kuhusu usahihi wa maudhui. HRT SACCOS haiwajibiki kwa hasara yoyote inayotokana na matumizi yako katika Tovuti hii.

7. Viungo kwa Tovuti nyingine

Tovuti yetu inaweza kuwa na viungo vya tovuti za taasisi zingine. HRT SACCOS Ltd haidhibiti maudhui ya tovuti hizo za taasisi zingine, hivyo basi HRT SACCOS haiwajibiki kwa maudhui yake.

8. Mabadiliko ya Vigezo na Masharti

Hai Rural Teachers SACCOS inahifadhi haki ya kufanya mabadiliko yoyote kwa Vigezo na Masharti haya wakati wowote. Mabadiliko yataanza kutumika mara tu yatakapochapishwa kwenye tovuti

9. Sheria Inayotumika

Vigezo na Masharti haya yatasimamiwa na kutafsiriwa kulingana na sheria za Tanzania. Mashauri yoyote yanayotokana na matumizi ya Tovuti hii yatatatuliwa chini ya sheria za Tanzania.

10. Mawasiliano

Kwa maswali yoyote kuhusu Vigezo na Masharti haya, tafadhali wasiliana nasi kupitia:

Barua Pepe: [email protected]

Namba ya Simu: +255 715 371 153

Anuani S.L.P 8, Hai, Kilimanjaro-Tanzania

Last updated: March 2026