Loading...

Kuhusu sisi

Sisi ni taasisi inayowawezesha Wanachama wake kufikia uhuru wa Kiuchumi kupitia huduma na bidhaa bora, ushauri wa kitaalamu, na ushirikiano wa karibu. Tunajenga maisha bora kwa kila Mwanachama, hatua moja baada ya nyingine.

kubadilisha maisha kupitia uwezeshaji wa kifedha

Chama kilianzishwa mwaka 2000, HAI RURAL TEACHERS SACCOS LTD ni Chama cha Ushirika cha Akiba na Mikopo (SACCOS) iliyosajiliwa kwa nambari ya usajili REG: PRI-KJR-HAI-DC-2022-1418. Kikihudumia wanachama kutoka Wilaya za Hai na Siha, Mkoa wa Kilimanjaro.

Kwa kipindi cha miaka mingi, tumekua kutoka taasisi ndogo hadi kuwa taasisi thabiti ya kifedha inayowahudumia Wanachama zaidi ya 3,000. Uwezo wetu wa kuwa wazi, kuwa na uadilifu, na kuwapa kipaumbele kwa huduma na bidhaa zinazolenga Wanachama wetu, ndio msingi wa mafanikio yetu hadi leo.

25+ Miaka ya Huduma
3,000+ Wanachama Hai
TZS 15B+ usimamizi wa mali
Hai Rural Teachers SACCOS Team

Dhamira Yetu

Kutoa suluhisho na ubunifu wa bidhaa na huduma bora zinazowawezesha Wanachama wa Wilaya za Hai na Siha kufikia uthabiti wa kifedha, ukuaji, na kujitegemea kupitia misingi ya ushirika na utekelezaji endelevu.

Dira Yetu

Kuwa chama cha ushirika bora kwa kutambulika kwa ubora wa huduma kwa wanachama, ubunifu wa bidhaa, na mchango wake katika maendeleo ya jamii ifikapo mwaka 2030.

Safari Yetu

Mafanikio na hatua muhimu zilizounda ukuaji na ustawi wetu

2000

Kuanzishwa

Hai Rural Teachers SACCOS ilianzishwa na Wanachama waanzilishi 67 waliounganishwa na dira ya pamoja ya kuwawezesha walimu Kiuchumi.

2001-2013

Ukuaji wa Haraka

Hai Rural Teachers SACCOS imepata ukuaji wa haraka kupitia ongezeko la wanachama na huduma bora za kifedha.

2014

Mabadiliko ya Kidijitali

Kutumia suluhisho za mifumo ya kibenki katika uendeshaji wa shughuli za kila siku

2020

Kasi ya Ukuaji

Tulifikia Wanachama 2,000 na kupanua wigo wa huduma na bidhaa zetu kujumuisha uwekezaji na mipango ya Kimkakati.

2020 - sasa

Ubora

Miongoni mwa SACCOS zinazofanya vyema Kilimanjaro na Tanzania kwa ujumla

Ifahamu Timu Yetu

Wataalamu wetu wanaojituma na wanaoendesha dhamira yetu kwa bidii na ufanisi

Mwl. Alex Warioba

Mwenyekiti

Mwl. Alex Warioba

Mwenyekiti

Mwl. Alex Ameleta uongozi wenye maono katika SACCOS yetu.

Mipango ya Kimkakati Uongozi Elimu
Sarah Kimambo

MS. Upendo Lyatuu

Mtendaji Mkuu

MS. Upendo Lyatuu

General Manager

Anasimamia na kuongoza shughuli zote za Chama, kuhakikisha utekelezaji wa mikakati, ukuaji endelevu, na mafanikio ya jumla. Anaongoza timu, anachangia maamuzi ya kimkakati, na kuhakikisha rasilimali zinatumiwa kwa ufanisi.

Fedha na mipango Uendeshaji Huduma kwa Wanachama
Godgift Kimaro

Godgift Gadiel Kimaro

Mhasibu Mkuu

Godgift Gadiel Kimaro

Mhasibu

Mhasibu anasimamia taarifa za fedha na kuhakikisha uwazi, usahihi wa taarifa, na ufanisi wa matumizi. Anaongoza timu ya kifedha na kusaidia kufanya maamuzi ya kimkakati.

Uhasibu Uwekezaji Usimamizi
Ernest Mziray

Ernest Mziray

Afisa Mikopo

Ernest Mziray

Afisa Mikopo

Anahusika katika mchakato mzima wa utoaji mikopo kwa Wanachama na ufuatiliaji wa marejesho. Anajitolea kutoa huduma bora za Mikopo, kusaidia Wanachama kufikia malengo yao ya kiuchumi, na kuhakikisha uwajibikaji na uendelevu wa Chama chetu.

Ufuatiliaji na Tathmini Uchambuzi wa Mikopo Usimamizi wa Fedha

Dhima za Msingi

Kanuni zinazotuongoza kwa kila kitu tunachokifanya

Uadilifu

Tunafanya kazi kwa uaminifu, uwazi, na uwajibikaji katika shughuli zetu zote.

Kuzingatia wanachama

Bidhaa na huduma zetu zinazingatia maslahi ya kila mwanachama kwa usawa.

Ushirikiano

Tunathamini kazi ya pamoja na tunahimiza ushirikiano kati ya wanachama, Viongozi na Watendaji kwa mafanikio ya chama chetu.

Ubunifu

Tunatafuta njia mpya na bora za kutoa bidhaa ili kukidhi mahitaji ya wanachama wetu.

Uwazi

Tunahakikisha taarifa zote na maamuzi ya chama yanatolewa kwa uwazi kwa wanachama wetu.

Uwajibikaji

Kuchukua jukumu kikamilifu kwa vitendo na maamuzi yetu, kuhakikisha matokeo yanalingana na ahadi na matarajio ya wanachama na jamii.

Uendelevu

Tunajitahidi kujenga taasisi imara na endelevu kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.