Hai Rural Teachers SACCOS (HRT SACCOS) imejizatiti kuhakikisha kwamba huduma, bidhaa, na miundombinu yake inapatikana kwa wanachama wote. Dhamira hii inatokana na imani yetu katika ushirikishwaji na lengo letu la kuwawezesha wanachama na jamii kupitia suluhisho bora kwa kuwapatia huduma bora
HRT SACCOS inajitahidi kila siku kuhakikisha huduma zake zinapatikana kwa urahisi kwa kila Mwanachama, wakiwemo Wanachama wetu waliopo nje ya Hai na Siha na wale walioko maeneo ya mbali. Hapa chini ni baadhi ya hatua tunazochukua kufanikisha hili:
HRT SACCOS inaendelea kupanua huduma zake kupitia ofisi kuu na tawi letu liloko Siha ili kuhakikisha wanachama waliopo wilaya ya Siha wanapata huduma kwa urahisi. Kila tawi limezingatia miundombinu rafiki kwa watu wenye ulemavu, ikiwemo milango mikubwa, sehemu za huduma zenye uwiano sahihi, na huduma rafiki kwa kila Mwanachama.
Tunatoa huduma kwa njia nyingi ili kuhakikisha kila Mwanachama anaweza kufikiwa kwa urahisi:
HRT SACCOS inaendesha mafunzo ya elimu ya fedha kwa wanachama wote kuhusu usimamizi bora wa fedha, uwekezaji, na faida za kuwa Mwanachama wa SACCOS.
Tunashirikiana na wanajamii, wanachama, na wadau mbalimbali ili kubaini changamoto za upatikanaji na kuzitatua kwa pamoja. Kupitia tafiti na maoni ya mara kwa mara, tunahakikisha huduma zetu zinabaki kuwa jumuishi na bora kwa wote.
HRT SACCOS itaendelea kuboresha upatikanaji wa huduma zake ili kila Mwanachama, bila kujali uwezo au eneo alipo, aweze kufurahia huduma zetu kwa usawa na kujikomboa kiuchumi.
Tunakaribisha wanachama wote kutembelea matawi yetu kwa huduma bora na rafiki:
Wilaya ya Hai, Mkoa wa Kilimanjaro
Kituo cha Wilaya ya Siha
Last Updated: March 2026