Mwanachama anaweza kuweka fedha zake katika akaunti hii kiasi chochote anachoweza kwa hali ya usalama na kuzichukua wakati wowote anapohitaji.
Chama kinatoa mikopo ya elimu, biashara, kilimo na ufugaji, ujenzi, ununuzi wa vyombo vya usafiri, viwanja na shughuli zote za maendeleo. Muda wa marejesho ni mwezi mmoja (1) mpaka miezi 60 kwa riba nafuu sana. Kiwango cha juu cha mkopo ni TZS 40,000,000 kwa Mwanachama mmoja
Mwanachama atanunua Hisa za msingi zisizopungua 70 sawa na TZS 700,000. (Thamani ya Hisa moja ni TZS 10,000) ili kumuwezesha Mwanachama kuwa mmiliki wa Chama. Mwanachama anaruhusiwa kununua Hisa za hiari (Zaidi ya TZS 700,000) ilimradi asizidi 20% ya Hisa zote za Chama.
Mwanachama ataweka Akiba kwenye Chama kuanzia TZS 25,000 kila mwezi kulingana na uwezo na mipango ya Mwanachama. Akiba hii itakuwa dhamana ya mkopo na Mwanachama atakopeshwa mara nne ya Akiba zake na kwa kupata faida ya asilimia 7-9 kwa mwaka. Akiba haitachukuliwa na Mwanachama mpaka uanachama unapokoma.
Mwanachama ataweka Akiba ya dharura kwenye Chama kiwango cha juu TZS 600,000. Akiba hii itakuwa dhamana ya mkopo wa dharura na atakopeshwa mkopo wa dharura mara 5 ya Akiba ya dharura.
Bidhaa zetu zinakidhi Mahitaji ya Wanachama wetu wote.
Furahia Mikopo ya Riba Nafuu kutoka Hai Rural Teachers SACCOS Ltd.
Fedha zako ziko salama na zimehakikishiwa kwa ulinzi wa juu ili kukupa utulivu na amani ya moyo
Hai Rural Teachers SACCOS Ltd husaidia katika kutatua changamoto, kuboresha maisha, na kukuza ustawi wa jamii kwa ujumla.
Jiunge na maelfu ya Wanachama wa HRT SACCOS Ltd ambao tayari wananufaika na kuwa na maisha bora kupitia bidhaa zetu ikiwemo mikopo ya Maendeleo, mikopo ya dharura, Mikopo ya salary advance, Kuweka akiba, kuweka amana ya muda Maalum